TANGAZO
Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania kinawatangazia
nafasi za kujiunga na Remedial Programme kwa
mwaka wa masomo 2012/2013.Kozi hii ni kwa ajili ya
wale wote ambao alama zao hazifiki kiwango cha 4.5
katika kidato cha sita, ili kuwawezesha kupata elimu ya ili
iwasaidie kuendana na wanafunzi wenzao waliopata
alama zaidi ya 4.5 katika kidato cha sita.
Sifa za Muombaji:
1. Awe amemaliza kidato cha sita.
2. Awe na Principal Passes 2 (mfano: EE, DE, CE, DD,
EEE na masomo mengine kuwa na S) ambazo
zinafikia 2.5 hadi 4 kwenye masomo mawili ya kidato
cha sita
3. Gharama ni Tshs. 390,000/= (Tuition Fee) kwa
miezi 3, malazi (accommodation) ni Tshs. 70,000/=,
chakula ni kujitegemea.
4. Wale wote wenye sifa hizo watakaochaguliwa na TCU
kuja SAUT watatakiwa kufika chuoni miezi mitatu
kabla ya tarehe ya kujiunga chuoni kwa ajili ya kuanza
masomo ya remedial.
5. Kozi hii itaanza tarehe 2/7/2012.
Fomu zinapatikana ofisi ya Admissions office na kwenye
tovuti (www.saut.ac.tz). Baada ya kumaliza kujaza fomu
zirudishwe ofisi ya Admissions-SAUT.
Wahitimu wataruhusiwa kujiunga na vyuo vyote vilivyo
chini ya SAUT ambavyo vinatoa programmes husika.
NB: WAOMBAJI PIA WANAPASWA KUOMBA KUPITIA
TCU
Wote mnakaribishwa.
Admissions Officer
No comments:
Post a Comment